KIKOSI chetu kitaondoka Tunisia mchana wa leo kwa Ndege ya Shirika la Emirates, na kutua Dubai saa 5:00 usiku.

Msafara utalala hapo Dubai na kesho, saa 3:30 asubuhi utaanza safari ya kurejea nyumbani ambapo tunatarijia kutua kwenye uwanja wa ndege wa Tanzania majira ya saa 1:55 mchana.

Kikosi kitarejea kuanza maandalizi ya mchezo wa pili wa makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa siku ya Jumapili tarehe 19, kwenye dimba la Benjamin Mkapa.