WANANCHI tumeanza vibaya kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF kwa kupoteza kwa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Monastir.

Mabao haya mawili yalifungwa ndani ya dakika 15 za kwanza kwa faida ya mipira ya juu iliyoingia ndani ya boksi la Yanga.

Matokeo haya yameifanya Yanga kukamata nafasi ya 4 kwenye msimamo wa kundi D, huku Mazembe wakiongoza kundi hili kwa pointi 3 baada ya ushindi wa mabao 3-1 walioupata dhidi ya Real Bamako.

Mchezo ujao wa Yanga utapigwa Jumapili kwenye dimba la Benjamin Mkapa, dhidi ya TP Mazembe.