KUELEKEA mchezo wetu wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF, dhidi ya Monastir siku ya kesho, kocha wetu mkuu, Nasreddine Nabi na mshambuliaji Fiston Mayele wamefanya mahojiano na Waandishi wa habari.

Mkutano huu na waandishi wa habari umefanyika kwenye ukumbi wa ndani ya uwanja wa Olympic Rades.

KUHUSU MAANDALIZI

“Nawapongeza sana viongozi wa Yanga kwa kuhakikisha timu inapata maandalizi mazuri hapa Tunisia. Tumekuwa na kambi nzuri sana hapa na vijana wako kwenye hali nzuri.

“Kuhusu maandalizi sisi tulishaanza tangu tukiwa Dar Es Salaam, tumefanya maandalizi mazuri na vijana wako tayari kwa ajili ya mchezo huu.

”Ni mchezo muhimu kwetu katika safari yetu ya kutafuta tiketi ya kwenda Robo Fainali ya michuano hii msimu huu,” alisema Nabi.

Kwa upande wa Mayele, alisema wachezaji wako tayari na morali iko juu sana kwenye timu.

“Tahadhari ni kubwa sana. Monastir ni wapinzani tofauti na Club Africain. Lakini morali ya kikosi iko juu sana na ninaamini tuna imani tutafanya vyema,” alisema Mayele.