BEKI mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi zote za pembeni, Shomari Kibwana amesema ujio wa beki Djuma Shabani na Joyce Lomalisa kutoka DR Congo, umemsaidia sana kuimarisha uwezo wake.

Kibwana ameyasema haya akiwa hapa Tunis, Tunisia, Yanga tukijiandaa na mchezo wa kwanza wa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF, dhidi ya Monastir.

Yanga itashuka kwenye uwanja wa Olympic Rades, siku ya Jumapili majira ya saa 1:00 kwa saa za Tanzania.

“Hawa wawili ni wachezaji wakubwa sana, ni jambo la kujivunia sana kama mchezaji unapopata nafasi ya kucheza ya wachezaji wakubwa katika timu moja, wananipa changamoto ya kupambana na kuwa bora siku zote,” alisema Kibwana.