RAIS wa Yanga, Eng Hersi Said leo asubuhi ameitembelea timu ya Royal FC inayoshiriki Ligi daraja la tatu kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mmoja wa wamiliki wa Royal FC, iliyoanzishwa mwaka huu, Ali Mohammed Bujsaim, miongoni mwa marefa wenye heshima kubwa duniani akiwa na rekodi ya kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia mara tatu [1994,1998,2022].

Mbali na rekodi hiyo, Bujsaim amechezesha pia Fainali Nne za Africa, [AFCON] na baadhi ya mechi kubwa Amerika Kusini.

Ziara ya Hersi kwenye klabu hii ni kutengeneza mahusiano mazuri kwa ajili ya kusaidia vijana wa Kitanzania kupata fursa ya kucheza soka kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu.

Hersi amebaki Dubai kwa ajili ya ziara hiyo ya siku 2 na atajiunga na kikosi cha Yanga, kwenye mji wa Tunis, hapa Tunisia, February 10.