MSAFARA wetu umetua salama kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tunisia, majira ya saa 8:40 mchana kwa saa za Tanzania.

Baada ya kuwasili, kikosi kilisubiri kwa saa 1:30 ndani ya uwanja wa ndege kwa ajili ya kukamilisha taratibu za VISA kisha kutoka na kuelekea hotelini.

Kikosi kimefikia kwenye hoteli ya Golden Carthroge na kwa mujibu wa taarifa ya benchi la ufundi, kikosi kitakuwa na session moja tu ya mazoezi ya utimamu wa mwili.