MSAFARA wa kikosi chetu ulifika salama Dubai majira ya saa 11:00 usiku jana, kwa saa za Tanzania na kufikia katika hotel ya Copthrone Hotel.

Baada ya kupata chakula cha usiku, kikosi kilipumzika hapa Dubai usiku wa jana na leo saa 2:00 asubuhi tunaanza safari ya kuelekea Tunis, Tunisia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Yanga itacheza na Monastir kwenye uwanja wa Olympic Rades, February 12, Jumapili hii ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Kundi D.