Mshambuliaji wetu wa Yanga Princess na Raia wa Nigeria, Blessing Nkor siku ya jana alifanikiwa kufunga magoli matatu “hatrick” kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) dhidi ya The Tiger Queens kwenye Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na YANGA MEDIA, Blessing alisema anasikia furaha kufanikisha hilo.

“Kwanza namshukuru Mungu kwa ushindi, Najisikia furaha sana kwa kufunga hatrick, pia namthamini mchango wa wachezaji wenzangu wa Princess kwa juhudi zao, ujasiri, umakini na uthubutu kwani bila wao nisingeweza”

“Nimeweka historia kwani hii ndio hatrick yangu ya kwanza kwenye maisha yangu ya soka” Blessing Nkor aliejiunga na Yanga Princess akitokea Sunshine Queens FC ya Nigeria , aliongezea.

Kuhusiana na namna anavyojisikia kuwa sehemu ya timu hii , Blessing anasema:

“Najisikia furaha sana kuwepo kwenye hii timu”

Baada ya mchezo huo, Blessing anakuwa mchezaji anaeongoza kwa magoli kwenye kikosi chetu kwa msimu huu, akiwa amefunga magoli manne mpaka sasa.