MCHEZO wa Ligi Kuu ya NBC kati yetu na KMC utapigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Februari 22,2023 majira ya saa 10:00 jioni.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo kama mgeni, itacheza mechi hiyo saa 10:00 jioni ili iweze kujiandaa na safari ya kuelekea Mali kwa ajili ya mchezo wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF, dhidi ya Real Bamako.

Yanga inatarajia kusafiri kuelekea Mali, Februari 23,2023.