JOPO la madaktari wa Yanga, likiongozwa na Daktari Moses Etutu waliokoa maisha ya abiria mmoja aliyepata changamoto ya afya ndege ikiwa angani.

Tukio hilo lililotokea ndani ya Shirika la ndege la Emirates, saa 2 kabla ya kutua nchini Tunisia.

Baada ya mgonjwa huyo kuwa kwenye hali mbaya, wahudumu wa ndege walitangaza kama kwenye ndege kuna mtu yoyote mwenye taaluma ya udaktari asimame kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Hapo ndipo madaktari wa Yanga walisimama na kuwahi kumpa huduma ya kwanza mgonjwa huyo aliyekuwa na changamoto ya sukari na maradhi mengine.

Wakati rubani wa ndege akifikiria kutua uwanja wa ndege wa karibu, Daktari Etutu aliwahi na kutoa huduma na hali ya mgonjwa huyo ikaimarika na ndege kuendelea na safari.