KIKOSI chetu kimeondoka kwenye uwanja wa ndege wa Julias Kambarage Nyerere kuelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Msafara huu utatua Dubai saa 3 usiku wa leo na kupumzika hapo kabla ya kesho saa 2 asubuhi kuanza safari ya kuelekea Tunis, utakapopigwa mchezo dhidi ya Monastir.