TIMU yetu ya wanawake Yanga Princess imeondoka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya The Tiger Queens kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (SWPL) uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam jioni ya leo.

Blessing Nkor akiwa kwenye kiwango bora kabisa aliifungia Princess magoli matatu na ikiwa ni hatrick yake ya kwanza, huku magoli mengine yakifungwa na Wogu Success pamoja na Nadege.

Ushindi huo umeifanya Princess kufikisha pointi 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake na kupanda kwenye nafasi ya kwanza kwa tofauti ya magoli.