Wakati Klabu ikielekea kwenye mchezo wa kwanza wa makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya US Monastir mchezo utakaopigwa tarehe 12 Februari kwenye dimba la Stade Olympique de Radès (Stade Olympique Hamadi Agrebi) jijini Tunis, maandalizi ya mchezo wa kwanza wa nyumbani dhidi ya TP Mazembe yameanza kushika kasi.


Katika mchezo huo utakaopigwa tahere 19 Februari majira ya saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, umepewa jina la WANANCHI SUPER SUNDAY, ikiwa ni kauli mbiu ya kuwaunganisha wananchi wote kwa pamoja kuipa nguvu klabu yao.


Maandalizi ya mchezo huo yameanza mapema kwa kutangaza viingilio rasmi na vituo vya kuuzia tiketi hizo, akiongea na waandishi wa habari mapema leo Afisa Habari wa klabu Ali Kamwe alisema:
“Tunajua umuhimu wa kushinda mechi za nyumbani, hivyo tunahitaji sana uwepo wa mashabiki kuwapa nguvu na kuwapa hamasa wachezaji wetu na ndio maana tunaanza kuuza tiketi mapema ili kila mtu apate fursa ya kushiriki”

Viingilio ya mchezo huo itakuwa kama ifuatavyo.,
VIP A – 30,000
VIP B – 20,000
VIP C – 10,000
Mzunguko (Kutoka Leo) -3,000
Siku ya Mchezo – 5,000.