NI MUDA WA KIMATAIFA. Ndio, ni wakati wa Klabu kubwa Tanzania kupaa kimataifa kwenda kuiwakilisha nchi yetu kwenye michuano ya CAF.

Yanga imepangwa Kundi D, hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF pamona na timu ya TP Mazembe kutoka DR Congo, Monastir ya Tunisia na Raeal Bamako kutoka Mali.

Mchezo wa kwanza wa Yanga kwenye hatua ya makundi D, utachezwa ugenini Februari 12, 2023 dhidi ya Monastir kwenye uwanja wa Olympic Rades.

Msafara wa Yanga kuelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo huo, unatarajia kuondoka Tanzania kesho saa 9:00 mchana kwa shirika la ndege la Emirates.

Msafara huo wa wachezaji 25, benchi la ufundi 9 na viongozi 9 utaondoka Tanzania na kutua Dubai saa 3:20 usiku, na utalala hapo.

Kesho saa 2 asubuhi kikosi kitaanza safari kutoka Dubai na kuelekea Tunisia.

Orodha kamili ya wachezaji watakaosafiri ni Djigui Diarra, Metacha Mnata, Erick Johora, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Kibwana Shomari, Farid Mussa, Mudathir Yahya, Zawadi Mauya, Yanick Bangala, Jesus Moloko, Khalid Aucho, Djuma Shabani, Fiston Mayele, Kennedy Musonda, Stephane Aziz KI, Joyce Lomalisa, Tuisila Kisinda, Salum Abubakar, David Bryson, Dickson Ambundo, Mamadou Doumbia, Clement Mzize.

Golikipa Aboutwaleb Mshery amesafiri pia lakini yeye anakwenda kwa sababu ya operesheni ya goti atakayofanyiwa nchini Tunisia.

Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi yeye alishatangulia Tunisia kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huu dhidi ya Monastir.