NYOTA wetu wawili wa timu ya wanawake ya Yanga Princess, Safiatu Salif na Atanhloeto Nadege wameitwa kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kirafiki.

Golikipa Safiatu amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana kwa ajili ya mechi mbili za kitafiki dhidi ya Benin na Ivory Coast zitakazopigwa mwisho wa mwezi huu.

Kwa upande wa Atanhloeto, maarufu kama Nado, yeye ameitwa kwenye timu yake ya Benin kitakachocheza dhidi ya Ghana na Togo.

Kikosi chetu cha Yanga Princess kitashuka kesho kwenye uwanja wa Uhuru, majira ya saa 10:00 jioni kuvaana na Tiger Queens, ukiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu ya Wanawake.