GOLIKIPA wetu Djigui Diarra mpaka sasa amefanikiwa kupata Clean Sheet 13, akiwa ni kinara kwenye orodha ya magolikipa waliocheza mechi nyingi bila kuruhusu bao.

Lakini kipa huyu wa kimataifa kutoka Mali anafukuzia rekodi yake ya msimu uliopita ya kucheza mechi 15 za Ligi Kuu bila kuruhusu bao.

Kiwango hiko cha CleanSheet kilimpa Diarra tuzo ya kuwa golikipa bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita.

Je, Diarra atavuka rekodi hiyo ya msimu uliopita? Ndio swali ambalo mashabiki wengi wa soka wamekuwa wakijiuliza wakati huu.