MABAO mawili aliyoyafunga kwenye mchezo dhidi ya Green Eagles yamemfanya mshambuliaji wetu anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Zesco United kufikisha idadi ya mabao matatu.

Huu ni mchezo wa pili kwa Kambole akiwa na Zesco na tayari amepachika mabao 3 kikiwa ni kiwango bora sana kutoka kwa Mzambia huyo.

Mabao hayo kwenye mchezo Green Eagles, Kambole aliyafunga katika dakika ya 60 na 92 na kuipa Zesco ushindi wa mabao 3-0.

Ikumbukwe Kambole yuko kwa mkopo Zesco kwa kipindi cha miezi sita.