MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, leo tutashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 12:30 jioni kuvaana na Namungo FC.

Yanga tunaingia kwenye mchezo huu tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-0 tulioupata kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi uliopigwa katika uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.

Kurejea kwa kiungo Khalid Aucho kutaipa nguvu zaidi safu yetu ya kiungo kwenye mchezo ambao ni wa mwisho kwenye Ligi kabla ya kuanza mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Mpaka sasa Yanga tunaongoza Ligi ya NBC tukiwa na pointi 56 huku Namungo wakikamata nafasi ya 6, wakiwa na pointi 29 huku timu zote zikicheza michezo 21.