MOTO wetu ni uleule kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu. Vichapo tu.

Hili limedhihirika kwenye mchezo wa leo dhidi ya Namungo FC ambako Yanga walipata ushindi wa mabao 2-0.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huu yalifungwa na nahodha Dickson Job kwa kichwa kikali akiunga krosi ya Djuma Shabani.

Bao la pili lilifungwa na kiungo wa kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kwa shuti kali akitumia makosa ya ya golikipa wa Namungo, Deogratius Munishi ‘Dida’.

Ushindi huu umeifanya Yanga kufikisha pointi 59 na kuzidi kujikita kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.