Daktari wa timu yetu, Moses Etutu ametoa taarifa ya maendeleo ya wachezaji wetu wawili Abutwalib Mshery pamoja na Bernard Morrison ambao walikuwa na majeraha tofauti.Akizungumza na YANGA MEDIA, Daktari Moses alisema kuwa kipa wetu Abutwalib Mshery atakuwa nje kwa takribani miezi 3-4.


“Mshery ana shida ya goti kitaalamu inaitwa “meniscus grade 2 tear” ambapo ataenda kufanyiwa upasuaji nchini Tunisia na baada ya hapo atarejea kwa ajili ya uangalizi wa karibu”
Daktari pia amezungumzia kuhusiana na Bernard Morrison ambae nae yupo nje kwa muda mrefu,


“Morrison ana shida ya nyama za paja (pubalgia) na atakuwa nje kwa muda wa miezi miwili, na ameshaanza kutibiwa mpaka sasa akiwa ameshakamilisha asilimia 40% ya matibabu yake”
Tunawatakia pole na kuwaombea warejee mapema kutoka kwenye majeraha yao.