TUMEINGIA hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam kwa kishindo kikubwa baada ya kuichapa Rhino Rangers kutoka Tabora kwa mabao 7-0.

Ushindi huu mkubwa zaidi kwenye hatua ya 32 bora umetufanya kupata rekodi ya kufunga jumla ya mabao 15 kwenye mechi mbili za Kombe la Shirikisho la Azam tulizocheza mpaka sasa.

Kwenye mchezo huu pia mashabiki wetu walishuhudia mshambuliaji Kennedy Musonda akifungua akaunti yake ya mabao baada ya kufunga mara 2.

Mabao yetu mengine kwenye mchezo huu yalifungwa na Dickson Ambundo, Yanick Bangala, Farid Mussa, David Bryson na Stephane Aziz KI aliyekuwa kwenye kiwango kikubwa sana.

Kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam, tutakutana na timu ya Tanzania Prison.