Uongozi wa Young Africans Sports Club umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mzee Shiraz Sharif, kilichotokea mchana wa leo, Januari 22, 2023.

“Hili ni pigo kubwa kwa familia ya michezo nchini, Yanga tutamkumbuka mzee Shiraz kwa mapenzi yake makubwa aliyokuwa nayo kwa klabu yetu. Unapotaja jina la Shiraz unakuwa umetaja jina la mwanachama wetu maarufu aliyefanya makubwa kwa Yanga kwenye miaka ya 1960,” Rais wa Yanga Eng. Hersi Saidi.

Mzee Shiraz atakumbukwa kwa uongozi wake kwenye nafasi tofauti tofauti ndani ya klabu ya Yanga pamoja na udhamini wake ikiwemo kuisafirisha timu kwenda nchi mbalimbali kwa ajili ya maandalizi.

Uongozi wa Yanga unatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na wadau wote wa michezo nchini pia tunawaombea wote kwa Mwenyezi Mungu wapate nguvu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

Amen.