TIMU yetu ya wanawake ya Yanga Princess itasafiri Dar Es Salaam siku ya Jumanne jioni kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo dhidi ya Baobab Queens.

Mchezo huo utapigwa siku ya Alhamis, majira ya saa 10::00 jioni kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Princess inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuiadhibu Alliance Queens kwa mabao 5-2 kwenye mchezo uliopita.

Mratibu wa Princess, Kibwana Matokeo amesema kuwa msafara wa watu 34 utaondoka Dar Es Salaam na Jumatano watafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Jamhuri.

Princess inakamata nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kuvuna pointi 7 katika michezo 4 waliyocheza mpaka sasa.