KUNA vita kubwa ya soka leo visiwani Zanzibar. Yanga dhidi ya Singida Big Stars, huu ni mchezo wa maamuzi.

Nani anafuzu hatua na nusu fainali? Nani anatoka? Timu zote zimefungana pointi kwenye kundi B baada ya kushinda mechi zao za kwanza dhidi ya KMKM.

Tofauti ni kwamba Singida Big Stars wako kileleni kwa faida ya tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa.

Mchezo wa kwanza wao walishinda mabao 2-0 na Yanga tukaichapa KMKM bao 1-0, bao lililofungwa dakika ya mwisho ya mchezo na winga Dickson Ambundo.

Matokeo pekee ambayo Wananchi wanayahitaji leo ni ushindi lakini kwa Singida Big Stars, hata wakipata sare ya aina yoyote, watakuwa na nafasi ya kusonga mbele.

Kila la kheri Yanga.