TIMU yetu ya wanawake Yanga Princess imeondoka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Alliance Girls ya Mwanza.

Mabao ya Yanga Princess kwenye mchezo huu yalifungwa na Maimuna Hamis, maarufu kwa jina la Mynaco, nahodha Amina Bilali, Wincate Kinyua na Aniella Uwimana aliyefunga mabao mawili.

Mabao ya Alliance Girls yalifungwa na Alia Fikiri na Fatuma Hassan kwa mkwaju wa penalti.

Ushindi huo umeifanya Princess kufikisha pointi 7 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake na kupanda kwenye nafasi ya 3 katika msimamo.