TIMU yetu ya wanawake ya Yanga Princess leo itashuka kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar Es Salaam majira ya saa 10:00 jioni kupambana na Alliance Girls.

Huu ni mchezo wa nne kwa Princess kwenye Ligi Kuu ya wanawake msimu huu, wakishika nafasi ya 5 baada ya kujikusanyia pointi 4.

Alliance Girls wako nafasi ya 4 wakiwa na pointi 7 baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare mchezo mmoja.

Princess wenyewe wameshinda mchezo mmoja dhidi ya Mkwawa Queens kwa bao 4-0, kisha kupata sare ya bao 1-1 kwenye Derby dhidi ya Simba Queens na wamepoteza kwa bao 1-0 mbele ya Fountain Gate.

Mchezo huu hautakuwa na Kiingilio na utaonyeshwa Mbashara kupitia YANGA APP na YANGA TV inayopatikana kwenye mtandao wa YouTube.