BAO la dakika ya 94 lililofungwa na winga Dickson Ambundo limeweza kutupa furaha Wananchi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMKM ya visiwani Zanzibar.

Ushindi huu ni wa kwanza kwa Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi 2023, na umetupa nguvu kuelekea mchezo wa pili wa Kundi B, dhidi ya Singida Big Stars.

Yanga inakamata nafasi ya pili kwenye kundi B tukilingana pointi 3 na Singida Big Stars lakini wana faida ya mabao mengi ya kufunga.

Kivutio kikubwa kwenye mchezo huu ni kiwango cha kinda Daruwesh na kiungo mpya Mudathir Yahya aliyeingia kipindi cha pili.

Mchezo unaofata ni dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa Januari 6, majira ya saa 2:15 usiku kwenye dimba la Amaan, hapa Zanzibar.