KIUNGO wa timu yetu ya Wanawake, Maimuna Hammis, maarufu kama ‘Mynacco’ amesema maandalizi yako vizuri kwa upande wa wachezaji kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Alliance Girls.

Akizungumza na YANGA MEDIA, Maimuna amesema mchezo wa kesho ni mgumu sana lakini kwa sapoti ya mashabiki wetu kwa kuja kwa wingi kuishangilia timu yetu itawasaidia kupambana na kubeba pointi tatu.

Yanga Princess itawakaribisha Alliance kesho kwenye uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 jioni na mashabiki watapata nafasi ya kuushuhudia mchezo huu bure kwani hakuna kiingilio.

Usisahau pia mpambano huu utaruka Mbashara kupita YANGA APP kuanzia saa 9:45 mchana.