WINGA Dickson Ambundo amewaomba mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars kwani wao kama wachezaji wamepania kufanya makubwa kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2023.

Ambundo mfungaji wa bao pekee la Yanga kwenye mchezo dhidi ya KMKM amekiri ugumu wa mashindano kwa mwaka huu lakini yeye anaona bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

“Mashabiki wazidi kutuamini na wajitokeze uwanjani kwa wingi, sisi tutapambana na tutafika fainali na kwa uwezo wa mwenyezi Mungu tutachukua kombe.

“Mashindano ni magumu, kila timu inaonekana kujiandaa vizuri lakini sisi Yanga tuna nafasi ya kupigana na kuondoka tukiwa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa mwaka huu,” alisema Ambundo.