NDIO. Ulichokisoma ni sahihi kabisa.

Achana na zile stori za kwenda wapi na wapi, Daktari wa mpira, Khalid Aucho ni mali ya Jangwani kwa mwaka mmoja zaidi.

Aucho alisajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili la mwaka 2021 na kusaini kandarasi ya miaka miwili akitokea klabu ya Makkasa SC ya nchini Misri.

Akiwa na jezi ya Wananchi, Aucho amekuwa nguzo muhimu kwenye safu ya kiungo ya Yanga na hii ndio imepelekea benchi la ufundi kuona kuna umuhimu wa kumuongeza mkataba.

Kama ilivyo siku zote, mchezaji mkubwa huchagua timu kubwa na Leo, Aucho ameichagua timu kubwa.