BAADA ya kuwasili kwenye visiwa vya Zanzibar jana jioni, kikosi chetu kitafanya mazoezi katika uwanja wa Mao, leo saa 10:00 jioni.

Yanga inatacheza mchezo wake wa kwanza kwenye Kombe la Mapinduzi kesho saa 2:15 usiku dhidi ya KMKM inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar.

Akizungumza na YANGA MEDIA meneja wa kikosi cha Yanga, Walter Harrison amesema wachezaji wana morali kubwa sana ya kufanya vizuri kwenye michuano hii.

“Tulifika hapa Zanzibar jana jioni na benchi la ufundi likashauri kikosi kipumzike na leo kuwe na ratiba ya mazoezi kwa kipindi kimoja.

“Kiujumla kikosi kiko kwenye hali nzuri na morali ya vijana iko juu sana. Tuna vijana hapa kutoka kikosi cha vijana ambao unaona kabisa wamejiandaa kushindana ili kuonyesha uwezo wao,” alisema Walter.