FISTON Kalala Mayele ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa DR Congo kwa mwaka 2022.

Tuzo hizo zimetolewa na mtandao mkubwa nchini DR Congo, Leopard Foot na Mayele kufanikiwa kuwabwaga wenzake kwa ushindi wa asilimia 81.

Akizungumza na YANGA MEDIA Mayele amesema ni jambo kubwa kwake kama mchezaji kushinda tuzo hiyo na ametoa shukrani zake kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kwa kuweza kumpigia kura.

“Nafurahi sana kushinda tuzo hii ya mchezaji bora wa mwaka wa DR Congo. Natoa shukrani zangu kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kwa kunipigia kura. Tuuanze mwaka 2023 kwa nguvu kubwa ya kuipambania timu yetu izidi kupata mafanikio,” alisema Mayele