BAADA ya Wananchi kusubiri sana, hatimaye vyuma vimeanza kutua. Na tunaposema vyuma, tunamaanisha vyuma kweli kweli.

Kiungo chuma, Mudathir Yahya ni mali ya Yanga baada ya Mzanzibar huyu kusaini mkataba wa kuwatumikia Wananchi.

Mkataba huo ulisainiwa mchana leo mbele ya Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said na mtendaji mkuu Andre Mtine

Baada ya kusaini mkataba huo, Mudathir alipanda boti na kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Yanga kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi.