MSAFARA wa wachezaji 24, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga watasafiri leo majira ya saa 10:00 jioni kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi 2023.

Kombe la Mapinduzi limeanza kutimua vumbi jana na Yanga tumepangwa Kundi B, pamja na timu ya Singida Big Stars na KMKM kutoka Zanzibar.

Wananchi tutashuka dimbani kucheza mchezo wetu wa kwanza wa Kombe hilo, tutacheza Januari 4, dhidi ya KMKM majira ya saa 2:15 usiku.