NYOTA Yusuph Athuman ametolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Coastal Union kwa kipindi cha miezi sita.

Yusuf alijiunga na kikosi chetu akitokea Biashara United msimu wa 2021/22, ameomba kutolewa kwa mkopo ili apate muda zaidi wa kucheza baada ya ushindani wa namba kuwa mkubwa kwenye kikosi cha Yanga.

Uongozi wa Yanga unamtakia kila la kheri mshambuliaji huyu katika majukumu yake mapya ndani ya Coastal Union ya Tanga.