KWAHERI mwaka 2022 na karibu 2023. Furaha iendelee kwa Wananchi.

Ndani ya mashamba ya miwa ya Manungu, kikosi cha Yanga tumeondoka na pointi tatu muhimu baada ya kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0.

Bao hilo pekee kwa Yanga kwenye mchezo huu lilifungwa kwenye dakika ya 26 kwa ‘Free kick’ kali iliyomshinda golikipa wa Mtibwa Sugar, Razack Shekimweri.

Ushindi huu umeifanya Yanga kufikisha pointi 50 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, tukiwaacha kwa alama 6 wapinzani wetu Simba SC wanaokamata nafasi ya pili.