KIKOSI cha Yanga kimewasili salama Turiani, utakapopigwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar, saa 10:00 jioni ya leo.

Timu itapumzika hapa na kupata chakula cha mchana na majira ya saa 8:00 mchana kikosi kitaanza safari ya kuelekea uwanja wa Manungu Complex.