Mshambuliaji wetu raia wa Jamuhuri Ya Demokrasia ya Congo (DRC), Fiston Mayele amesaini mkataba mpya kutumikia Young Africans SC mpaka mwaka 2024.

Mayele aliesajiliwa msimu wa 2021/22 akitokea klabu ya AS Vita amekuwa moja ya wachezaji muhimu katika kikosi cha mwalimu Nasreddine Nabi,ambae kwa msimu wake wa kwanza alifanikiwa kupachika magoli 16 na assists 5 kwenye ligi kuu ya NBC.

Tangu kuwasili kwake amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ngao ya Hisani, Kombe la Azam FA, na taji la Ligi Kuu ya NBC 2021/22.