WINGA wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Tuisila Kisinda amerejea Jangwani kwa mara nyingine.

Nyota huyo aliwahi kuitumikia Young Africans SC msimu wa 2020/21 kabla ya kusajiliwa na klabu ya Berkane ya nchini Morocco ambapo alifanikiwa kutwaa kombe la Shirikisho Afrika.

Tuisila anasifika kwa mpira wake wa kasi na chenga nyingi, ambao ulimpatia umaarufu mkubwa alipokuwa akicheza ligi kuu ya Tanzania bara.

Kisinda anakuwa mchezaji wa mwisho kusajiliwa na Young Africans SC baada ya dirisha la usajili kufungwa usiku wa tarehe 31 August, na kukamilisha idadi ya wachezaji 6 waliosajiliwa kukiongezea nguvu kikosi hicho cha mabingwa hao wa ligi kuu ya NBC mwaka 2021/22.

Karibu tena Tuisila Kisinda “TK Master”