Young Africans SC imecheza mchezo wake wa pili ugenini, ikiwa pia ni mechi ya pili kucheza kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta.

Mchezo ulianza kwa kasi huku Yanga wakiwa wanaonesha nia ya kupata goli la mapema. Dakika ya 4 ya mchezo, Bernard Morrison alimalizia kwa uzuri pasi kutoka kwa Jesus Moloko na kuitanguliza Yanga kwa bao 1-0 mapema kabisa.

Mchezo ulikuwa una presha kubwa na kupelekea kutokea kwa fouls nyingi, dakika ya 20 ya mchezo, Jesus Moloko alichezewa vibaya na beki wa Coastal Union na kumsababishia maumivu yaliopelekea kutolewa dakika chache baadae na kuingizwa Dickson Ambundo. Kipindi cha kwanza kiliisha kwa Yanga kuwa mbele kwa goli moja.

Kipindi cha pili, Yanga waliendeleza kasi ile ile huku wakiwa na umiliki mkubwa wa mpira. Dakika ya 67, kupitia kona iliopigwa na Bernard Morrison ilimkuta Djuma Shaaban aliemtengea mpira Fiston Mayele alieuunganisha kwa kichwa na kuiandakia Yanga goli la 2.

Coastal Union licha ya jitihada zao za kurudisha magoli hayo, safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa imara kuzuia mashambulizi hayo.  Mchezo uliisha Yanga ikiibuka na ushindi wa goli 2- 0.

Baada ya mchezo huo baadhi ya wachezaji wetu wataungana na wenzao kwenye kambi ya Timu ya Taifa kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya CHAN, na wengine wataendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Azam FC, tarehe 6 Septemba.

Kikosi Kilichoanza:. Mshery, Djuma, Kibwana,/Lomalisa (dk 83) Bangala Mwamnyeto, Aucho, Feisal, Morrison/Farid (dk72) , Aziz Ki / Bigirimana (dk83) Moloko/Ambundo (dk20) Makambo /Mayele (dk55)

Subs:Johora, Job,Bacca,Mauya,Bigirimana,Ambundo,Lomalisa,Mayele