Kikosi Kilichoanza:. Diarra, Djuma, Lomalisa,Job,Mwamnyeto,Aucho,Bigirimana,Ambundo,Aziz Ki,Moloko, Mayele
Subs: Mshery, Bangala,Bacca,Feisal,Sureboy,Morrison,Farid,Makambo, Mauya.
Tumefungua pazia la Ligi Kuu ya NBC kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Polisi Tanzania ambao wametumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama mbadala wa uwanja wao wa Ushirika ulio kwenye marekebisho.
Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikiwa zinaonesha kusoma mchezo. Dakika ya tisa tu, Jesus Moloko aliangushwa kwenye box na muamuzi kuamuru iwe penalty. Fiston Mayele alishindwa kupeleka mpira nyavuni baada ya kipa wa Polisi kuupangua.
Mchezo uliendelea kwa kasi na dakika ya 33, Bakari Mwamnyeto katika harakati za kuokoa mpira ulimgonga mchezaji wa Polisi, Ally Salum Ally na kuelekea nyavuni na kuwatanguliza kwa goli moja.
Dakika ya 41 Yanga walisawazisha kupitia Fiston Mayele ambae aliemalizia mpira uliokuwa kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha pili kilianza kwa mwalimu kufanya mabadiliko, akimtoa Gael Bigirimana na kumuingiza Feisal Salum, na kumtoa Dickson Ambundo na kumuingiza Bernard Morrison. Mpira uliendelea kwa kasi huku Yanga wakitawala mpira kwa muda mwingi. Mwalimu aliendelea kufanya mabadiliko na kumtoa Jesus Moloko na kumuingiza Hertier Makambo. Dakika ya 84, Bakari Mwamnyeto alimalizia krosi safi ya Bernard Morrison na kufanya Yanga kuwa mbele kwa 1-2.
Juhudi za Yanga kuongeza goli la tatu ziligonga mwamba baada ya kosa kosa nyingi, pamoja na goli la Mayele kukataliwa na muamuzi.
Mechi Iliisha kwa ushindi wa goli Polisi 1-2 Yanga.