Leo mapema wanachama wawakilishi wa matawi yaliokidhi vigezo walikusanyika kwenye ukumbi wa JNICC ili kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wapya watakaoiongoza klabu kwa miaka minne ijayo.

Katika uchaguzi huo, Eng. Hersi Said alipitishwa bila kupigwa na wanachama wote katika nafasi ya Urais wa Klabu.

Katika nafasi ya Makamu Rais waliogombea nafasi hiyo walikuwa QS. Suma Mwaitenda Pamoja na Arafat Haji.

Ambapo Arafat Haji achaguliwa kuwa Makamu wa Rais Young Africans SC baada ya kupata kura 545 dhidi ya kura 234 alizopata mpinzani wake, Suma Mwaitenda.  Waliopiga kura walikuwa 785 na kura zilizoharibika zilikuwa ni sita (6)

Katika nafasi ya wajumbe wa kamati tendaji wafuatao ndio walipata kura nyingi: