Baada ya timu kukabidhiwa kombe jijini Mbeya,ilifika siku ya kulileta jijini Dar Es Salaam. Mapokezi ya timu yalipambwa na shughuli mbalimbali ambazo zilifana.  Sherehe hizo ambazo zilisimamisha jiji la Dar Es Salaam kwa muda kwa kutembea na basi la wazi ambalo lilikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa Yanga. Timu ilipokelewa kwenye makao makuu ya klabu, Jangwani na kulionesha kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza kwa wingi. Siku ilihitimishwa jioni yake amabapo kulikuwa na sherehe rasmi za ubingwa kwenye viwanja vya GSM, Samora. Baadhi ni picha mbali mbali za siku hiyo.