Viingilio vya mchezo wetu wa kwanza hatua ya awali katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O ya Burundi, vimetajwa.

Mchezo huo ambao tutacheza Jumamosi ya wiki hii saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Vital’O ndio watakuwa wenyeji kikanuni.

Kiingilio cha juu katika mchezo huo ni Tsh 50,000 kwa VIP A, wakati VIP B ni Tsh 30,000 na Mzunguko Tsh 10,000.

Baada ya mchezo huo, marudiano ni Agosti 24, 2024 huku tukiwa wenyeji ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua inayofuatia.