KIKOSI chetu cha Yanga SC, kimeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Al Merrikh, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza uliochezwa leo Jumamosi Septemba 16, 2023 kwenye Uwanja wa Pele Kigali, Rwanda.
Katika mchezo huo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mabao ya Yanga yalifungwa na Kennedy Musonda dakika ya 60 na Clement Mzize dakika ya 79.
Baada ya mchezo huo, kikosi chetu cha Yanga kinatarajiwa kurudiana na Al Merrikh Septemba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mchezo huo wa marudiano, kikosi chetu kinahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Ikumbukwe kwamba, Kabla ya kukutana na Al Merrikh, Yanga SC hatua ya awali iliibuka na ushindi wa jumla wa magoli 7-1 dhidi ya ASAS Djibouti.