Kikosi cha wachezaji wetu kimewasili jijini Dar Es Salaam kikitokea Dubai ambapo waliwasili jana usiku wakitokea nchini Tunisia ambapo walicheza mchezo wa kwanza wa makundi wa Kombe La Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir.

Timu baada ya kurejea wameelekea moja kwa moja kambini Avic Town ambapo wataanza na maandalizi kuelekea mchezo wa pili wa makundi dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa tarehe 19 siku ya Jumapili, siku iliopewa jina rasmi “WANANCHI SUPER SUNDAY”

Viingilio na vituo vya kufanyia mauzo  ya tiketi hizo vimeshatangazwa, mwananchi nunua tiketi yako mapema tukutane kwa Mkapa.