Wachezaji wetu wataanza kuripoti rasmi AVIC Town,Kigamboni- Dar Es Salaam kuanzia tarehe 20 July kujiunga na kambi rasmi ya kujiandaa na msimu wa 2022/23.
Kukiwa na baadhi ya wachezaji kwenye majukumu ya timu ya Taifa, kikosi kilichosalia na wachezaji wapya waliowasili wataanza maandalizi ya msimu mpya wiki hii kwa kufanyiwa vipimo kadhaa vya kimwili,kiafya na kuanza program maalumu ya kuupa mwili utimamu.
Kambi ya kujiandaa na msimu mpya (Pre-Season) huipa timu ya ufundi fursa ya kufanya tathmini kadhaa na kuandaa hali ya wachezaji kabla ya msimu kuanza.
“Tulipanga likizo yetu kumalizika tarehe 15/07/22 Makocha wakashauri tuwaongezee Wachezaji wetu muda wa mapumziko kwasababu walikuwa na msimu mrefu na hawakupata nafasi ya kupumzika kutokana na majukumu ya Klabu na timu za Taifa” alisema msemaji wa Klabu, Haji Manara kwenye mkutano na waandishi wa habari mapema leo.
“Wananchi” watatumia muda huo kujiandaa kabla ya kutangazwa kwa ratiba na tarehe za msimu mpya wa 2022/23.